Psalms 125

Usalama Wa Watu Wa Mungu

Wimbo wa kwenda juu.

1 aWale wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni,
ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele.
2 bKama milima inavyozunguka Yerusalemu,
ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake
sasa na hata milele.

3 cFimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi
waliopewa wenye haki,
ili wenye haki wasije wakatumia
mikono yao kutenda ubaya.

4 dEe Bwana, watendee mema walio wema,
wale walio wanyofu wa moyo.
5 eBali wale wanaogeukia njia zilizopotoka,
Bwana atawafukuza pamoja na watenda mabaya.

Amani iwe juu ya Israeli.
Copyright information for SwhNEN